Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro amefanya ziara ya kiserikali katika Jimbo la Songea Mjini kuanzia tarehe 09 Julai 2024 na kuhitimisha tarehe 17 Julai 2024 iliyofanyika kata kwa kata kwa lengo la kupokea Kero mbalimbali za Wananchi.
Katika ziara hiyo Dkt. Ndumbaro aliambatana na Wataalamu mbalimbali kutoka Sekta ya Elimu, Afya, Mipango miji, Uchumi, Kilimo, Tasaf, TARURA, TANROAD, SOUWASA, viongozi wa vyama vya Siasa, na Waheshimiwa Madiwani ambapo amefanikiwa kukamilisha kutembelea kata zote 21 za jimbo la Songea Mjini.
Miongoni mwa kero nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza kwenye kata hizo ni pamoja na changamoto ya miundombinu ya Barabara, Vivuko na mifereji, ukamilishaji wa miundominu ya ofisi za Serikali za mita, miundombinu ya Elimu Msingi, Umeme, na Maji,
Wakitoa majibu kupitia wataalamu walioshiriki ziara hiyo ambapo walisema miongoni mwa kero za miundombinu iliyotajwa imetengewa bajeti katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2024/2025 ili kupunguza au kuondoa kabisa changamoto hizo
Akihitimisha ziara hiyo katika kata ya Subira ambapo amewataka wananchi wa Manispaa ya Songea kuendelea kuwa na subira wakati Serikali ikiendelea kutatua changamoto za Wananchi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa