Halmashauri ya Manispaa ya Songea kupitia baraza la Madiwani Manispaa ya Songea wameweka mikakati madhubuti ya kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa lengo la kuongeza mapato kutoka Bil 6 hadi Bil. 15 kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya Halmashauri hiyo.
Katika kutekeleza mikakati hiyo Madiwani, viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya, pamoja na wataalamu wamefanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya Chalinze na Tanga Jiji kwa lengo la kwenda kujifunza nmna ya uendeshaji wa miradi ya kimkakati pamoja na ukusanyaji wa mapato ya madini ya ujenzi.
Ziara hiyo imefanyika kuanzia tarehe 06 hadi tarehe 10 Aprili 2024 ambapo walitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ambako walijifunza namna ya uendeshaji wa miradi ya kimkakati, ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia madini ya ujenzi ambayo ni chanzo kikubwa cha mapaoto cha Halmashauri hiyo ambacho kinawezesha kuongeza mapato kwa asilimia 60% ambapo huweza kukusanya mapato Bil. 15 kwa mwaka.
Akizungumza Naibu Meya Manispaa ya Songea Jeremiah Mlembe “ Lengo la ziara hiyo ni kujifunza katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ambayo imeanzishwa mwaka 2016 lakini katika ukusanyaji wa mapato wamefikia hatua ya kukusanya Bil. 15 kwa mwaka ikiwa ni mapato ambayo 60% yanatokana na madini ya ujenzi. “ aliwapongeza.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komredi Oddo Mwisho alisema” Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kupitia viongozi wake wamekuwa bega kwa bega kuhimiza Manispaa ya Songea iweze kuwa Jiji na ili iweze kuwa Jiji ni lazima ikusanye mapato makubwa ambayo yatawezesha wananchin kupata huduma.
Akizungumza mheshimiwa Mbunge wa Viti ,Maalumu Jacqueline Msongozi alitoa shukrani kwa uongozi wa Manispaa ya Songea kwa kuandaa ziara ya kwenda kujifunza nmna ya ukusanyaji wa mapato ya madini ya ujenzi ambayo yanasaidia kukuza mapato ya Halmashauri .
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa