Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano amewataka wataalamu pamoja na Madiwani kutumia elimu ya mafunzo waliyoipata iweze kuboresha ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kuongeza kiwango cha mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Kauli hiyo imetolewa kwenye ziara ya Madiwani na wataalamu walipotembelea Jiji la Tanga iliyofanyika trehe 09 April 2024 kwa lengo la kujifunza namna walivyofanikiwa ukusanyaji wa mapato ya Halmashaurai hiyo.
Mhe. Mbano alisema “ Zipo ndoto za Manispaa ya Songea kuwa Jiji endapo mapato yatakusanywa kama ilivyokusudiwa yatawezesha kufungua fursa nyingi za uwekezaji na kunufaisha jamii ya kanda ya kusini . “Alisisitiza”
Akizungumza Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abrahman Shilow “Tumeguswa na ziara yenu kwasababu ziara hiyo itasaidia kuboresha utendaji wa kazi baina ya Manispaa ya Songea na Jiji la Tanga. “ Aliwakaribisha”
Kwa upande wake Mkurugenzi Manispaa ya Songea Adv. Bashir Muhoja alisema Nanukuu ”Tumefanikiwa kufanya ziara katika Halmashauri mbili tofauti ambapo Halmashauri ya Chalinze tumejifunza namna yao ya ukusanyaji wa mapato ya madini ya ujenzi ambapo kwa mwaka 2023/2024 Halmashauri ya Chalinze wamekisia kukusanya Bil. 15. Mwisho wa kunukuu”
Adv. Muhoja aliongeza kuwa, Katika Halmashauri ya Jiji la Tanga wamejifunza namna ya ukusanyaji wa mapato ya madini ya ujenzi ambapo Halmashauri hiyo kwa mwaka 2023/2024 imekisia kukusanya mapato kiasi cha Bil. 19,145.700,000.
Alisema, ili kufanikisha ukusanyaji wa mapato hayo inahitaji ushirikishwaji, kuwawezesha wakusanyaji wa mapato ikiwa ni sehemu ya kuwatia moyo ili waweze kukusanya mapato kwa kiasi kikubwa . “ Alibainisha.”
Kwa upande wa Madiwani walitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea kwa kuandaa ziara ya mafunzo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia vyanzo mbalimbali vya madini ya ujenzi na namna ya usimaiaji wa miradi ya Kimkakati inayotekelezwa kwenye Halmashauri hizo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa