Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dkt. Frank Walter Steinmeier amewataka Watanzania wote kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kudumisha ushirikiano na uhusiano baina ya nchi mbili kati ya Ujerumani na Nchi ya Tanzania.
Kauli imetolewa katika viwanja vya makumbusho ya Taifa ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji iliyofanyika leo tarehe 01 Novemba 2023 kwa lengo la kukumbuka historia ya Tanzania na Ujerumani yenye taswira mbili ambayo iliwafanya Watanazia wateseke.
Dkt. Frank amesema nanukuu, Ameguswa sana na historia ya familia Nduna Songea Mbano ambayo imetolewa na kupitia taarifa hiyo imewezesha kupata ufahamu wa jambo la kinyama ambalo lilifanywa na Majeshi ya Wajerumani ambalo ni la kusikitisha na hatimaye ameweza kufika mji wa Songea na kupata historia ya babu zenu. Mwisho wa nukuu.
Alisema amejifunza mambo mengi ikiwemo na Shujaa wa Kingoni ambaye alitawala kwa Mila za kingoni pia alikuwa kiongozi shujaa wa vita vya Majimaji ambaye alitawala kwa ushujaa sana ambapo alihaidi kuwa upande wao ili waweze kutawala na baada ya kupinga majeshi ya wajermani walinyongwa na kuzikwa katika kaburi moja lenye watu 69.
Aidha, Watanzania watakumbuka kuwa mabaki ya wanadamu yaliweza kusafirishwa na kupelewka ujerumani hata hivyo amewahakikishia kuwa kichwa cha Nduna Mbano watajitahidi kutafuta japokuwa ni vigumu kufahamu mabaki ya mwili wa binadamu.
Hata hivyo, aliomba Msamaha kwa yaliyotokea pamoja na familia ya Mbano kwa yale yote yaliyofanywa na majeshi ya Ujermani huku akiiniamisha kichwa chini kwa ajili ya Kuomboleza pia akisisitiza kuendelea kuwepo kwa Mahusiano kati ya Mji wa Songea na Ujermani pamoja na shule ya Msingi Majimaji ambayo ina jina la kumbukumbu wa mashujaa wa vita vya Majimaji.
Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro (MB) amesema lengo kuu ni kukumbuka historia ya Tanzania na Ujermani, amayo ilitokana na kumalizika kwa vita vya majimaji tarehe 27 februali ya mwaka 1905 pamoja kuleta mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Ujermani na kufuta historia mbaya ya awali ya Ujermani.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa