Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Ahmed Abbas Ahmed amewataka wataalamu wa Manispaa ya Songea kusimamia kwa ukaribu miradi ya maendeleo inayojengwa ili iweze kukamilika kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa tarehe 29 Mei 2024 akiwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya uboreshaji wa Miundombinu ya barabara za lami KM 10.1 zilizopo katikati ya Mji ambayo ilifanyika kwa lengo la kufanya ufutailiaji wa hatua za mradi husika.
Akizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Wakili. Bashir Muhoja alisema “Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 12 zilizo bahatika kupata mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara za lami nzito KM 10.1 inayojumuisha barabara 20 za katikati ya mji zinazotengenezwa kupitia mradi huo.
Alisema mradi huo umefadhiliwa na jumuiya ya maendeleo ya kimataifa (IDA) kupitia Benki ya dunia kwa ajili ya kuboresha miundombinu na ushindani wa Miji, Manispaa, na Majiji nchini Tanzania (TACTIC) ambao unaratibiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Kupitia timu ya uratibu wa miradi (PCT) ambao umeanza tarehe 20 Novemba 2023 na kumalizika tarehe 6 Februali 2025 kwa gharama ya mradi Mil. 938,395,000 ambao upo asilimia 8.3 kati ya 40.5 ya utekelezaji wa mradi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa