Na. AMINA PILLY
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA
Kiongozi wa Mbio maalmu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021, Ndugu yetu Luteni Josephine Paul Mwambashi, amezindua na kukagua jumla ya Miradi 4 yenye thamani ya Shilingi 1,464,246,586 Halmashauri ya Manispaa ya Songea ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu pamoja na nguvu za wananchi.
Luteni Mwambashi ameweza kuzindua na kukagua miradi minne ndani ya Manispaa ya Songea ambapo miradi miwili ni uzinduzi ambayo ni mradi wa maji Lilambo A na B wenye thamani ya shilingi 1,164,555,586/=, pamoja na mradi wa Barabara uliopo mtaa Ruhila kata ya Seedfarm wenye thamani ya shilingi 294,691,000/=.
Aidha miradi mingine miwili iliyotembelewa na Mbio Maalmu za Mwenge wa Uhuru ni pamoja na Mradi wa upandaji Miti Mitiki 10,000 uliopo Mtaa wa Sinai Kata ya Lilambo wenye thamani ya shilingi Milioni 5,000,000/= pamoja na Kituo cha kutolea Elimu na huduma ya Tehama kilichopo Soko kuu Songea Mjini.
Mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru 2021 zimeadhimishwa kiwilaya ambapo jumla ya miradi 9 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.2 iliwekwa mawe ya msingi, kufungua, kuzindua, na kukagua.
Kauli mbiu za Mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru 2021, ni TEHAMA ni “msingi wa Taifa Endelevu Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji”, ambapo katika kutekeleza ujumbe wa mwenge wa Uhuru ambao pia uliamabatana na ujumbe wa MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI “Mshikamano wa Kitaifa Tuwajibike kwa pamoja”, MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA “Ziro Malaria inaanza na Mimi nachukua hatua kuitokomeza”.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema alianza kwa kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuenzi Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazofanyika kila mwaka, kwani zinasaidia kufanya Wananchi wa Songea kuwa na umoja, amani, utulivu, upendo, mshikamano na maendeleo ya hali ya juu pale unapopita Mwenge.
Mwenge wa uhuru umepokelewa tarehe 06 septemba katika kijiji cha Liganga Halmashauri ya Wilaya ya Songea na kukabidhiwa Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe 07 septemba 2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa