IBARA ya 76 ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi katika Ibara ndogo ya 4 Ukurasa namba 76 wa katiba umetamka Kazi na Majukumu ya Halmashauri Kuu ya chama ikiwemo na Kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo, kusimamia na kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa.
Aidha, mabadiliko ya katiba mpya imeongezwa majukumu ya Halmashauri kuu ya Kata ambayo imeeleza katika Ibara ya 50 katika Ibara ndogo ya 4 Ukurasa namba 43 umewataka kutekeleza majukumu ngazi ya Kata, Wilaya hadi Mkoa, hata hivyo utekelezaji wa maagizo hayo unatakiwa kutekelezwa kuanzia sasa.
Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Mwenyekiti wa CCM Songea Mjini Hamisi Abdallah Ally ameongoza kikao maalmu cha Utekelezaji wa Ilani ambacho kilihudhuriwa na wajumbe wa Halmshauri kuu ngazi ya Kata kilichofanyika tarehe 14 Septemba 2022 katika Ukumbi wa CCM tawi la Songea Mjini kwa lengo la kupokea taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mkuu wa Wilaya.
Hamisi amewataka viongozi wa vyama vya siasa wasiwe sehemu ya walalamikaji katika maeneo yao bali wawe viongozi wafuatiliaji wa shughuli zote zinazofanywa na Serikali ili kuondoa malalamiko kwa wananchi wanaowaongoza.
Aliongeza kuwa kila kiongozi anapaswa kutambua miradi yote inayotekelezwa na Halmashauri katika maeneo wanayoishi na kujijengea tabia ya kufanya ziara mara kwa mara kwa lengo la kukagua mradi na kufahamu muda wa kuanza kwa mradi, ukomo wa utekelezwaji wa mradi na gharama za mradi husika ili waweze kuisemea Serikali kwa wananchi. Alisisitiza
Ametoa rai kwa wataalamu wa TARURA kuchonga barabara chache zenye viwango vinavyotakiwa kulingana na mpango na bajeti iliyowekwa na kuacha kuchonga barabara nyingi chini ya kiwango kwa ajili ya kuwanufaisha viongozi wa vyama vya siasa kitendo ambacho kinaathiri miundombinu ya barabara na kusababisha malalamiko kwa wananchi.
Hamisi, amewataka wataalamu wa kilimo kutumia pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa kuwatembelea wakulima mashambani pamoja na kufanya upimaji wa udongo ili wakulima waweze kulima kilimo chenye tija.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wote kwa kuchaguliwa katika chaguzi mbalimbali zilizofanyika hivi karibuni kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, na Kata na kuwataka kila mmoja katika nafasi yake atekeleze wajibu wake.
Oddo alibainisha kuwa jambo muhimu katika chama cha mapinduzi ni kuendelea kudumisha Ushirikiano ndani ya chama, kuimarisha Chama kiuchumi, kisiasa, na kuendelea kujitegemea kwa kuanzisha miradi mipya au kuendeleza miradi iliyopo.
Akisoma taarifa hiyo Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ni Kuhakikisha kwamba halmashauri zote nchini zinaendelea kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kwa mujibu wa sheria ili kuwezesha vijana na makundi mengine katika jamii zetu kupata mikopo isiyo na riba.
Pololet alisema kuwa Katika kutekeleza maelekezo ya Ilani kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ilifanikiwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya makusanyo kwenda kwenye akaunti ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiasi cha tshs 356,700,000.00 hadi kufikia septemba, 2022 jumla ya tshs 250,000,000.00 kimetolewa kwenda kwenye akaunti ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu sawa na asilimia 70.08 ya lengo.
Alisema Mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia TASAF awamu ya III kipindi cha kwanza ulianza kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016, ambapo jumla ya mitaa 53 imenufaika na mpango huu, hadi sasa jumla ya kaya 5,618 zimenufaika na Mpango huu wa kunusuru kaya maskini.
kipindi cha mwezi Julai hadi septemba, 2022/2023 Halmashauri inaendelea na ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa na mabweni 2 katika shule ya Wasichana ya Songea na vyumba 3 vya madarasa na mabweni 2 katika shule ya wavulana Songea. Ujenzi wa miradi hii upo katika hatua mbalimbali, ambapo gharama za ujenzi wa miradi hii inayoendelea ni Tshs. 540,000,000.00
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa