Kauli hiyo imetamkwa na Afisa mwandamizi Idara ya Uanachama Mkoa wa Ruvuma Katondo Gideon katika kikao cha Watumishi Sekta ya Elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea leo 09.09.2020.
Katondo alisema MTBA ni taasisi ya Umma iliyoundwa kwa mujibu wa Sheria Na. 8 Sura Na. 395 TL 1999 na Utekelezaji wake ulianza Julai 2001 ambayo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya mabadiliko katika Sekta ya Afya (1990s), kwa lengo la kutoa Bima ya Afya kwa makundi mbalimbali kwa wananchi, kujenga uwezo wa kipato kwa vituo, kushirikisha sekta binafsi katika kuharakisha maendeleo katika sekta binafsi.
Alisema Mfuko wa Bima ya Afya unamilikiwa na Serikali kwa 100% na unasimamiwa na Bodi ya Wakurugenzi inayojumuisha wadau muhimu Nchini. Dhana ya Bima ya Afya imejengeka katika misingi ya mshikamano wa kijamii katika kuchangiana gharama za matibabu.
Alibainisha kuwa Mtumishi huchangia 6% ya mshahara wake wa mwezi kwa usawa kati ya mwajiri 3% na mwajiriwa 3% na kuwa na jumla ya Wanufaika ni sita (6) na iwapo mume na mke ni wachangiaji idadi ya Wanufaika ni (10) ambao pia Wanufaika ni mwanachama mchangiaji, mwenza wake, watoto wa kuzaa au kuasili, wake/wakwe ikiwa pamoja na uwasilishaji wa nyaraka za uthibitisho. Alisistiza.
Aliongeza kuwa Katika kuongeza uwigo wa Wanachama wake, Mfuko umeanzisha huduma mpya ambayo ni Toto Afya Kadi (Watoto wa ziada wanaweza jumuishwa katika utaratibu huu), Wanafunzi, Ushirika Afya (wakulima kupitia AMCOS), Madereva Bodaboda, Vifurushi vya bima (Najali, Wekeza na Timiza.
Alisema huduma za matibabu hupatikana popote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ni zaidi ya vituo 8,022 vinavyotoa huduma za matibabu bila kujali hali ya afya au kiasi cha mchango pamoja na huduma za matibabu kwa mwanachama mstaafu na mwenza wake katika maisha yao yote.
Katondo akitaja mafao yatolewayo na Mfuko wa Bima ya Afya nipamoja na ada ya uandikishaji na ushauri wa tiba, huduma ya wagonjwa wa nje, huduma ya Dawa zaidi ya aina 975, huduma ya wagonjwa wa ndani, huduma za Vipimo mbalimbali, huduma za matibabu ya kinywa, huduma za upasuaji wa aina zote (moyo, mifupa, mishipa ya fahamu etc).
Aidha, katika kikao hicho kuliibuka na malalamiko kutoka kwa Watumishi hao wakilalamikia Mfuko wa Bima ya Afya kuwaondoa wanachama ambao wamefikia au kuzidi umri wa miaka 18 bila kujali kama ni wanafunzi wa shule. Naye Afisa mwandamizi wa Uanachama Mkoa wa Ruvuma Katondo Gideon alisema nanukuu “ hiyo ni sheria ambayo ilishatungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwahiyo ipo kwenye utekelezaji wake, lakini pia aliahidi kuchukua maoni /ushauri wote na kuyawasilisha ngazi ya juu.” Mwisho wa kunukuu.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa