Siku ya wauguzi duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 12 Mei ya kila mwaka ambapo kwa manispaa ya Songea sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Bustani ya Manispaa ya Songea tarehe 31 Mei 2024.
Siku hiyo iliibuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1953 na Dorothy Sutherland aliyekuwa Afisa kutoka kitengo cha elimu ya afya na Ustawi huko U.S ili kuangalia mchango wa wauguzi katika kuhudumu jamii ambapo baraza la Wauguzi ulimwenguni (International Council of Nurses) ilianza kuadhimisha siku hiyo tangu mwaka 1965 na mwaka 1974 mwezi januari lilipotolewa tamko rasmi kuwa siku ya wauguzi Duniani iadhimishwe ulimwenguni kote kila ifikapo tarehe 12 Mei kila mwaka.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Bi Ziada Sella Mkurugenzi Huduma za Ukunga Wizara ya Afya ambaye amewataka wauguzi wote kuendelea na utaratibu wa kufanya kazi za kutoa huduma za kijamii bure na isiishie kwenye maadhimisho bali iwe endelevu.
Katika kuadhimisha sherehe hizo wauguzi waliendesha zoezi la utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii bila malipo yoyote ikiwemo na kutoa huduma ya upimaji wa VVU, kutoa huduma ya uzazi wa mpango, na kufanya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi.
Aidha, ikisomwa risala na Roda Mtung’e afisa muuguzi Msaidizi alisema wanaishukuru Serikali kwa jitihada zinazofanyika za kuboresha mazingira ya huduma za afya ikiwemo na kujenga Hosptali ya Manispaa ya Songea, Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa jamii. Walishukuru.
Kauli Mbiu ya mwaka huu 2024 ni;
Wauguzi; Sauti ya kuongoza – wekeza katika uuguzi na heshimu haki linda Afya.
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa