Katibu Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, itikadi, Uenezi na Mafunzo Paulo Makonda amewataka viongozi wote Mkoani Ruvuma kufanya kazi kwa kufuata misingi na haki katika kuwahudumia wananchi ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 10 Februari 2024 akiwa ziarani Mkoani Ruvuma ambapo aliweza kuhutubia wananchi katika uwanja wa Matarawe ambayo walishiriki waheshimiwa Wabunge Mkoani Ruvuma, viongozi wa vyama vya siasa, pamoja na wananchi iliyofanyika kwa lengo la kusikiliza kero kutoka kwa wananchi hao.
Makonda, akitoa salaamu za pole kutoka kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema “ Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeungana na Mwenyekiti wa CCM kuipa pole familia ya Hayati Ngoyai Edward Lowasa na wanachama wote wa CCM kwa kumpoteza kiongozi mpendwa ambaye katika uhai wake alitoa mchango mkubwa katika Taifa kupitia nafasi zote alizohudumu enzi za uhaai wake.
Chama Cha Mapinduzi kinaungana na watanzania wote katika kuomboleza msiba wa Hayati Ngoyai Edward Lowasa aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu ambaye amefariki tarehe 10 Februari 2024 saa nane mchana katika Hospitali ya Moyo Muhimbili.
Aidha baaada ya salamu hizo za pole kwa famialia na watanzania wote, katibu mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kisha kutoa ufafanuzi kulingana na hoja ziliulizwa na kisha alitoa agizo kwa uongozi wa Mkoa kuitisha kikao cha kupokea kero ili kutatua changamoto za wananchi hao.
Ziara hiyo imekuwa ni muendelezo wa ziara katika mikoa mbalimbali ambayo anaendelea kufanya.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa