Manispaa ya Songea imeendelea kupokea wageni kutoka nje Mkoa wa Ruvuma wakifika katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji na usimamizi wa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kwa mara nyingine tarehe 22 Mei 2023 Manispaa ya Songea ilipokea Waheshimiwa Madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambao walikuja kwa lengo la kujifunza namna inavyoendeshwa na kusimamia machinjio ya kisasa ya Songea ikiwemo na tozo, na kiutawala.
Akizungumza Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwada alisema Manispaa ya Iringa ina machinjio ambayo bado haijakamilka japokuwa imeanza kufanya kazi na huchinja katika mfumo ambao sio wa kisasa.
Mhe. Ngwada alisema kupitia hilo walipendekeza kuja Manispaa ya Songea ili kuboresha utendaji wa kazi pia kuendelea kuweka mahusiano ya ki-Halmashauri hasa ikiwa inaendesha miradi inayofanana ni muhimu ujifunze kupitia wengine.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano aliwakaribisha wageni hao na kisha kuwaongoza katika kila hatua ya uendeshaji wa mradi wa Mchinjio ya kisasa iliyopo kata ya Tanga Manispaa ya Songea.
Naye Mkurugenzi Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko alianza kwa kuwakaribisha wageni kisha alieleza Mradi huo umegharimu kiasi cha Bil. 5.7 na umeanza kutoa huduma japokuwa bado haujakamilika kwa asilimia 100%.
Alisema kuwa mfumo wa uchinjaji nyama katika machinjio hiyo ni wa kisasa ambao unatumia mtambo ambapo Manispaa ya Songea ni miongoni mwa miji michache nchini Tanzania ambayo inatumia mtambo huo.
Dkt. Sagamiko aliongeza kuwa kupitia machinjio ya kisasa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea yameongezeka ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 walikisia kukusanya kiasi cha Mil 379.
Kwa upande wa waheshimiwa Madiwani walisema wamejifunza mambo mengi kupitia ziara yao na kujifunza namna mtambo wa kisasa unavyofanya kazi, miundombinu, sambamba na uwepo wa kichomeo cha wanyama ambao hawafai kwa kuliwa na mwanadamu. “Walishukuru”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa