NA; “Amina Pilly.”
Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wanawake, Wazee na Watoto Dkt. Mwanaidi Hamisi anaendelea na Ziara Mkoani Ruvuma ambapo ataweza kutembelea chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale, Hospitali ya Mkoa Songea (HOMSO) na Halmashauri nyingine kwa ajili ya kufanya uhamasishaji wa wazee ili waweze kujitokeza kupata chanjo ya kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19.
Dkt. Mwanaidi alisema hayo akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma jana 11 Agost 2021 kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli za Wazee na ustawi wa Jamii ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Mkakati wa Maendeleo ya jamii ya 1996, Wanawake na jinsia ya mwaka 2000 na Sera ya maendeleo ya mtoto ya mwaka 2008, Sera ya Taifa ya mashirika yasiyo ya Kiserikali 2001 na Sera ya Wazee 2003.
Miongoni mwa maeneo aliyoweza kutembelea ni pamoja na Hospitali ya Mkoa ambapo aliweza kukagua Chumba maalumu kwa ajili ya matibabu kwa wazee, Chumba maalumu kwa ajili ya Chanjo ya UVIKO 19, kisha kuchomwa chanjo hiyo kwa lengo la kuhamasisha wakazi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na Wazee kuweza kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo hiyo, pia ametembelea Shirika lisilo la kiserikali ROA pamoja na kikundi cha wananwake Malkia wa Nguvu kilichopo Kata ya Mjimwema ambapo alitoa zawadi ya rollu tano za kamba kwa ajili ya kutengenezea makapu ya kikundi hicho.
Dkt. Mwaaidi amepongeza Shirika la lisilo la kiserikali ROA kwa jitihada walizozionyesha za kuwafikia wasichana 3201 kwa kuwapatia elimu ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia, na kuimarisha ulinzi na ustawi kwa wananchi.
Amewataka wananchi Mkoani Ruvuma kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi ya UVIKO 19 kwa kunawa maji tiririka, kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa, pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyo na lazima.
Naye mwenyekiti wa ROA Mathew C.N. Ngalimanayo alisema “ ROA ilianzishwa ili kushughulikia masuala ya ustawi na maendeleo ya makundi yaliyo katika hatari ya kuathrika/kuathiriwa na umaskini na magonjwa.
Ngalimanayo aliongeza kuwa dhamira ya ROA inalenga kubuni, kupanga na kutekeleza mipango inayolenga kuwafikia, kuwasaidia, kuwaokoa na kuwaendeleza watu walio katika hatari ya kuathirika/kuathiriwa na umaskini na magonjwa kwa kushirikiana na wananchi, Serikali na wadau wengine.
Miradi hiyo imeweza kushughulikiwa katika maeneo makuu ambayo ni pamoja na Kinga dhidi ya VVU/UKIMWI, Huduma za VVU/UKIMWI majumbani (CBHS), Unasihi na upimaji wa VVU/UKIMWI kwa hiari, Ukatili wa kijinsia, Kujenga uelewa kwa jamii kuhusu Uzazi wa Mpango ambapo Mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri tano za Mkoa wa Ruvuma ambazo ni (Songea MC, Songea DC, Mbinga TC, Mbinga DC na Nyasa DC).
Aliongeza kuwa mradi wa USAID Boresha Afya unatekelezwa kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo ambapo Shirika la “Deloitte Tanzania” kwa mwaka 2020/2021 tumesaini mkataba wa Tshs. 890,000,000.00 ambapo kati ya fedha hizo Tshs. 10,260,000.00 ziliingizwa kwenye akaunti ya ROA na Tshs. 879,740,000.00 zinalipwa kutoka Ofisi ya Mfadhili moja kwa moja kwa walengwa.
Akibainisha changamoto zinazoikabili taasis hiyo ni pamoja na Ukosefu wa fedha za kutosha za kuendesha shughuli za Shirika kadiri ya malengo yao, Ongezeko kubwa la walengwa wanaohitaji huduma tofauti na rasilimali zliizopo, Kutofanikiwa kuwa na mradi wa moja kwa moja wa matunzo na misaada kwa Watoto yatima na Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, Ugumu wa usimamiaji na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za mradi wa Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI unaofadhiliwa na “Deloitte Tanzania” kwa sababu ya utaratibu wa mfadhili kuhodhi kiasi kikubwa cha fedha.
Alisema Mradi umeweka mpango wa utekelezaji kwa kutoa misaada na matunzo kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, Kuwezesha Kiuchumi Familia zenye watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, Kujenga na kuimarisha uelewa kwa Jamii juu ya haki na wajibu wa watoto, Kushirikiana na Serikali na wadau wengine kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa mpana juu ya masuala ya ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto.
AFISA HABARI - MANISPAA YA SONGEA.
12 AGOST 2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa