KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Meja Generali Gaudance Milanzi (pichani ) amewataka wadau mbalimbali wa utalii nchini, kulilinda ziwa Nyasa kwa kuwekeza katika sekta ya Utalii kutokana na ziwa hilo kuwa na vivutio adimu vya utalii ambavyo bado havijaendelezwa ukilinganisha na uwekezaji uliofanywa katika ziwa Nyasa upande wa nchi ya Malawi.
Akizungumza na watumishi wa Idara yake katika mkoa wa Ruvuma kwenye ukumbi wa Hunt Club mjini Songea, Meja Generali Milanzi amesema hakuna sababu ya kulinda ziwa Nyasa kwa kutumia silaha nzito badala yake ziwa hilo linaweza kulindwa kwa kufungua milango ya uwekezaji na utalii.
Ziwa Nyasa linaongoza Duniani kwa kuwa na aina zaidi ya 400 wa samaki wa mapambo ambao hawapatikani katika sayari nyingine yoyote Ulimwengu,ziwa hilo pia linaongoza duniani kwa kuwa na fukwe bora za asili,visiwa,mawe ya ajabu na vivutio vingine kama kuzungukwa na milima ya Livingstone stone.
Imeandikwa na Albano Midelo
Simu 0784765917,baruapepe albano.midelo@gmail.com
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa