TUKIWA tunaelekea katika tamasha la utalii na uwekezaji katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma ambalo linatarajia kuanza Januari Mosi 2019 na kilele chake Januari 6,2019.Hebu tuendelee kuangalia fursa adimu za utalii na uwekezaji zinazopatikana katika wilaya ya Nyasa.
Kulingana na utafiti ambao ulifanywa na Jumuiya ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika(SADC) kwa kushirikiana na nchi ya Uingereza kwenye ziwa Nyasa kati ya mwaka 1991 hadi 1994 na mwaka 1996 hadi 2000,ulionesha kuwa ziwa hilo lina kiasi cha tani 165,000 za samaki wa aina mbalimbalii.Ziwa Nyasa lina aina 1500 za samaki,zikiwemo aina zaidi ya 400 za samaki wa mapambo .Ziwa Nyasa limezungukwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania,Malawi na MsumbIji.Ziwa hilo lipo kwenye usawa wa meta 500 toka usawa wa bahari ambapo kina cha ziwa hilo ni karibu meta 750,urefu wake ni karibu kilometa 1000 , upana mkubwa ni kilometa 80 na upana mdogo ni kilometa 15.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa