UTAFITI umebaini ziwa Rukwa linandelea kusinyaa kwa kasi kila mwaka kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu.Utafiti uliofanywa mwaka 2013 na 2014 ulibaini kuwa ziwa Rukwa lilikuwa na wastani wa kina cha juu cha maji cha mita tisa na kina cha chini ni mita nne.
Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1970 hadi 2006 Ziwa Rukwa limepungua kwa kiasi cha zaidi ya kilomita saba.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba anasema mwaka 2000 kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita,ambapo mwaka 2016 kina kimepungua hadi kufikia mita tatu tu.
Ili kuyanusuru mazingira ya nchi yetu ni lazima hatua za makusudi zichukuliwe kudhibiti uharibifu wa mazingira unaoendelea. Hii ndio sababu Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuyafanya masuala ya hifadhi na usimamizi wa mazingira kama sehemu ya mhimili wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu.
Katika kulinda mazingira ya nchi yetu na kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira nchini, Ofisi imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Mikakati na Mipango mbalimbali ya hifadhi ya mazingira na mikataba ya kimataifa ya mazingira, pamoja na utoaji wa elimu kwa umma kuhusu mazingira. Hatua hizi zinalenga kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali ili kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii .
Mwandishi ni Albano Midelo simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa