DIRA YA HALMASHAURI YA AMANISPAA YA SONGEA. Halmashauri ya Manispaa ya Songea inakusudia kuwa na mji uliopangika, miundombinu ya kisasa, ongezeko la kipato na mwananchi mwenye maisha bora na endelevu kwa kudumisha ulinzi na usalama, usafi wa mji, uadilifu, uwazi, uzalishaji bora kuelekea kukuza Manispaa kuwa jiji. MWELEKEO WA HALMASHAURI YA MANISPAA. Halmashauri ya Manispaa ya Songea inatarajia kutoa huduma bora za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wake kwa kutumia fursa na rasilimali kuhamasisha, kuiendeleza, kuimarisha na kujasilisha wananchi katika mazingira ya ushindani na ubadilishaji wa rasilimali na huduma endelevu kwa kuzingatia sayansi, teknolojia, utandawazi na soko huru kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu bila kuathiri mila, desturi na utamaduni kwa umakini na ufanithi mkubwa kwa kutumia utawala bora ili kuinua au kuboresha hali za kimaisha kwa kuongeza uzalishaji na mauzo ya bidhaa, kukusanya mapato kwa njia ya kieletroniki, kuwa na miradi ya uzalishaji yenye tija, utendaji wenye maadili na nidhamu kwa kuzingatia kauli mbiu. Nawasalimu kwa jina la JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa