KAMATI ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri hiyo.Hapa Kamati hiyo imetembelea mradi wa karakakana ya Halmashauri iliyopo Kata ya Misufini.
SHIRIKA lisilo la kiserikali la USAID PROTECT limetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi shilingi milioni 46 katika chuo cha mafunzo ya Uhifadhi wa maliasili (CBCTC) kilichopo Likuyu wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Mwakilishi wa USAID Thadeus Binamungu kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudence MilanziVifaa vilivyokabidhiwa ni jenereta moja,vionambali 10,GPS 10,Kompyuta mpakato tano,powerpoint mbili, na vitabu 40 kwa ajili ya kozi ya waongoza watalii.
JUMLA ya vijana 55 wamehitimu kozi ya miezi mitatu ya Askari wanyamapori vijijini(VGS) katika chuo cha Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii(CBCTC) kilichopo Likuyu Sekamaganga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.Mgeni rasmi katika mahafali hayo ambayo yamefanyika Juni 24,2018, alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudence Milanzi.Moja ya mambo ambayo yamemvutia zaidi ni ukrukwaji wa vikwazo kwa stahili ya Chimpanzee.Tazama mwenyewe
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa