WALIMU katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambao walipata barua za kupandishwa madaraja na bado hawajarekebishwa mishahara yao wameomba kuvuta subira kwa kuwa serikali kila mwezi inarekebisha mishahara ya walimu waliopandishwa vyeo.Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa hiyo Lewis Mnyambwa amesema majina ya walimu wote ambao walipandishwa madaraja yao katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 yameingizwa kwenye mfumo na kwamba kila mwezi kuna baadhi ya walimu ambao wanarekebishiwa mishahara yao.Amesema katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea idadi ya walimu waliopata barua za kupandishwa madaraja ni 704 na kwamba idadi hiyo ni kubwa hivyo walimu wanatakiwa kuwa na subira kwa kuwa serikali imekuwa inarekebisha mishahara yao kila mwezi.
JUMLA ya shilingi milioni 22 zimetumika kwa ajili ya kukamilisha maabara katika shule ya sekondari ya Matogoro iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Mkuu wa shule hiyo Ezra Mwogela amebainisha kuwa kati ya fedha hizo,shilingi milioni 17 zimetumika kwa utengenezaji na uwekaji wa samani za maabara na shilingi milioni tano zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa maabara.
KATIKA nchi ya Thailand kuna mapacha wawili ambao wameungana na hivi sasa wana umri wa miaka tisa.Mapacha hao wanaishi kijiji cha Nakhon kilometa 250 kaskazini mwa mji Mkuu wa Thailand,Bankok,wanaishi na wazazi wao.Madaktari bingwa katika nchi hiyo waliwafanyia uchunguzi watoto hao na kubaini kuwa wanaweza kufanyiwa upasuaji na kutenganishwa kisha kuendelea na maisha yao.
Hata hivyo mapacha hao walikataa kutenganishwa kwa kuwa wanaamini ni mapacha ambao wana nguvu kubwa wakiwa wameungana. Watoto hao walizaliwa kila mmoja akiwa kichwa chake na viungo vingine huku wakichangia baadhi ya viungo watazame.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa