MTAZAME Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akitoa maagizo mazito kwa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwenye kikao maalum cha kujibu hoja za ukaguzi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Pamoja na mambo mengine Mkuu wa Mkoa ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kuweza kupata Hati inayoridhisha mara mbili mfululizo na kusisitiza kuwa mafanikio hayo yasiwafanye wakajisahau kwa kuwa ukaguzi wa mahesabu unafanyika kila mwaka hivyo kujiandaa na ukaguzi ujao kwa kupunguza hoja.
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko ameutaka uongozi wa kampuni ya TANCOAL inayochimba madini ya makaa ya mawe katika machimbo ya Ngaka yaliyopo wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kufanya kazi kwa kufuata sheria
MKUTANO wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma limeunga mkono kusitisha nia ya kuanzisha Bodi ya Mfuko wa Elimu katika Manispaa hiyo.Mbunge wa Songea mjini Dk.Damas Ndumbaro akizungumzia sakata hilo,amesema lengo la rasmu hiyo lilikuwa ni kuboresha lakini kwa upande wa pili lilikuwa linagusa mfuko wa wananchi na kwamba limeleta dosari katika manispaa ya Songea
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa