MPAKA kufikia Juni, 2018, upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefikia asilimia 50.1 sawa na idadi ya watu 45,929 kwa wakazi waishio pembezoni mwa Mji wa Manispaa ya Songea yaani sehemu ambazo Mamlaka ya Maji safi na Taka (SOUWASA) hawajaweza kutoa huduma ya Maji safi na Salama.
Mkuu wa Idara ya Maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mhandisi Samwel Sanya anasema Halmashauri mwaka 2007 wakati inaanza kutekeleza programu ya maji ilikuwa na asilimia 17 tu na kwamba tangu mwaka 2007 inaendelea Kutekeleza Programu ya maji na Usafi wa Mazingira katika Mitaa 10 ,awamu ya kwanza ambayo ni Mahilo, Chandarua, Muhombezi, Muungano, Mahinya, Ngandula, Ruhuwiko Kanisani, Mitendewawa, Ruhila kati na Liwumbu.
TAZAMA yaliyojiri katika Mkutano wa Baraza Maalum la madiwani kuwasilisha Taarifa ya Hesabu za kufunga mwaka 2017/2018,kikao ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji
IKIWA ni takribani wiki moja imepita hadi sasa tangu umeme wa Grid ya Taifa ulipowashwa katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amezidua kiwanda kipya kilichojengwa katika kata ya Ruhuwiko Manispaa ya Songea chenye uwezo wa kusaga mahindi tani 30 ambayo ni sawa na magunia 300 kwa siku.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji akizungumza katika mkutano wa Baraza maalum la madiwani wa Manispaa hiyo wenye lengo la kuwasilisha taarifa za Hesabu za kufunga mwaka 2017/2018,amesema kiwanda hicho kimezinduliwa wakati muafaka kwa sababu hivi sasa kitapunguza changamoto za soko la mahindi katika manispaa ya Songea na mkoa wa Ruvuma na kutoa ajira kwa vijana.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa