Kampeni ya Furaha Yangu katika Mkoa wa Ruvuma inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 31 mwaka huu kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya,Ustawi Jamii,jinsia,watoto na wazee Ummy Mwalimu.
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameagiza hadi kufikia Septemba 30 mwaka huu vikundi vyote ambavyo bado havijalipa mikopo Yao waliochukua kupitia Benki za CRDB na TPB tawi la Songea wachukuliwe hatua za kisheria.Akizungumza kwenye kikao cha ufuatuliaji wa madeni kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea,Mndeme amesema Baraza la Taifa la Uwezesheji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Linadai vikundi,vyama vya ushirika na SACCOS zaidi ya shilingi milioni 197 ambazo walikopeshwa kupitia CRDB na TBP mkoa wa Ruvuma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na Wenyeulemavu Jenista Mhagama Tafiti zinaonesha kuwa hadi sasa ni asilimia tano tu ya watanzania wameambukizwa virusi vya UKIMWI ambapo asilimia 95 ya watanzania bado wapo salama.Kutokana na takwimu hizo Waziri Mhagama anasisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa asilimia 95 ya watanzania ambao bado jawajaambukizwa virusi vya UKIMWI wanalindwa ili wasipate na asilimia tano ya watanzania ambao wameambukizwa wanahudumiwa ili kufubaza virusi vya UKIMWI.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa