Mkurugenzi wa Kampuni ya TOPONE LIMITED ambao ndiyo wamiliki wa Chuo hicho Pascal Msigwa amesema chuo hicho kinatarajia kufunguliwa Oktoba mwaka huu ambacho kwa kuanzia kitakuwa kinatoa mafunzo ngazi ya cheti ambayo yanachukua miaka miwili.Msigwa amesema chuo hicho kimesajiriwa na Baraza la Ufundi la Taifa (NACTE) na kupewa namba ya usajiri 184 na kwamba lengo la kuanzisha chuo hicho kuiunga mkono serikali ya Awamu ya tano ya kuzalisha watalaamu wa ufamasia hapa nchini ili kukabiliana na upungufu uliopo.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kwa kufanikiwa kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria ambao unaongoza Tanzania kwa kusababisha vifo.
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametoa ametoa maagizo na maekezo kwa watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma.Ametoa maagizo hayo wakati anatoa Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 kipindi cha Julai, 2017 hadi Juni ,2018 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho,Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Profesa Riziki Shemdoe,Wakuu wa Wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma,watalaam ngazi ya Mkoa,viongozi na wajumbe mbalimbali wa CCM Mkoa wa Ruvuma
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa