SERIKALI za Mitaa katika Halmashauri za Wilaya,Miji,Manispaa na Majiji zimekuwa zinatambua,chambua na kuamua njia halisi na sahihi za kusaidia jitihada za jamii katika ngazi ya vitongoji,vijiji,mitaa na kata.
Mchumi Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,Raphael Kimary anazitaja njia kuu ya kutumia njia shirikishi ni kutokana na ruzuku au fedha ya kutegemea serikali ni kidogo.Alikuwa akizungumza kwenye mafunzo ya jitihada za jamii katika kuchangia miradi ya maendeleo ambayo yametolewa kwa madiwani wa Halmashauri hiyo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
MTAZAME Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea ambaye pia ni Diwani wa Kata ya subira Abdul Hasan Mshaweji anasema nia ya Halmashauri ni kusaidia jitihada za wananchi kwa kuwapa moyo na kuendeleza uwezo wa jamii hivyo ameshauri wadau wengine kushirikishwa ili kuchangia badala ya kusubiri serikali ambayo haina fedha za kutosha kutekeleza miradi.Alitoa maoni mara baada ya kupata mafunzo ya jitihada za jamii katika kuchangia miradi ya maendeleo yaliyoshirikisha madiwani wote wa Manispaa ya Songea Juni 29,2018.
WALIMU katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambao walipata barua za kupandishwa madaraja na bado hawajarekebishwa mishahara yao wameomba kuvuta subira kwa kuwa serikali kila mwezi inarekebisha mishahara ya walimu waliopandishwa vyeo.Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa hiyo Lewis Mnyambwa amesema majina ya walimu wote ambao walipandishwa madaraja yao katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 yameingizwa kwenye mfumo na kwamba kila mwezi kuna baadhi ya walimu ambao wanarekebishiwa mishahara yao.Amesema katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea idadi ya walimu waliopata barua za kupandishwa madaraja ni 704 na kwamba idadi hiyo ni kubwa hivyo walimu wanatakiwa kuwa na subira kwa kuwa serikali imekuwa inarekebisha mishahara yao kila mwezi.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa