KAMATI ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Songea imefanya ziara ya kukagua stendi mpya mabasi katika eneo la Kata ya Tanga nje kidogo ya Manispaa ya Songea.Mara baada ya ukaguzi kamati imeridhishwa na hatua ya ujenzi unaofanywa na Kampuni ya China Sichuan International.mradi umeanza Mchi 25,2018 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2018.Mradi unagharimu zaidi ya bilioni sita ambapo tayari mradi umefikia asilimia 14.
MTAZAME Kaimu Mhandisi wa Ujenzi katika Manispaa ya Songea Nicholus Danda akielezea awamu ya pili ya ujenzi wa stendi ya Tanga Manispaa ya Songea kwa Kamati ya Fedha na Uongozi ambayo ilitembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi wa stendi hiyo.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea kupitia program ya maji na usafi wa mazingira inaendelea kukarabati visima vya maji 89 lengo ni kuongeza utoaji huduma ya maji kwa wananchi.Mradi huo unaotekelezwa katika kata 10 unagharimu zaidi ya shilingi milioni 294.Hadi sasa visima 61 vimekarabatiwa bado visima 28.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa