MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema serikali imetoa fedha za mradi wa upanuzi wa barabara ya Songea hadi Makambako ili kuhakikisha miundombinu ya Barabara katika mkoa wa Ruvuma inakuwa ya kisasa.
Mimba za utotoni bado ni changamoto kubwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari katika mkoa wa Ruvuma. Takwimu zinaonesha kuwa katika wilaya ya Songea hadi kufikia mwezi Novemba 2018, wanafunzi 61 wamepata mimba na kukatisha masomo yao ambapo katika wilaya ya Namtumbo wanafunzi 69 katika shule za sekondari wamepata mimba na kushindwa kuendelea na masomo yao . Changamoto ya mimba za utotoni sio kwa mkoa wa Ruvuma pekee bali mikoa yote nchini ambapo Mkoa wa Shinyanga ndiyo unaongoza.
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amekagua mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya kata yake, Ruvuma manispaa ya Songea na kiridhishwa na kasi ya ujenzi wake .Ujenzi wa Kituo hicho ambacho serikali imetoa shilingi milioni 400, umeanza Septemba mwaka huu.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa