MWENYEKITI wa Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma Vestus Mfikwa amewaahidi wakazi wa kijiji cha Ifinga kuwa serikali katika mwaka mpya wa fedha wa 2018/2019 imetenga bajeti ya kutosha kuhakikisha kuwa sehemu korofi katika barabara hizo zinafanyiwa matengenezo makubwa .Amesema kijiji hicho pia kitafungukiwa huduma ya mawasiliano ya simu na kwamba hivi sasa mikataba dhidi ya kampuni ya simu ya hoteli imesainiwa na baada ya mwezi mmoja mkandarasi anatarajia kuanza kujenga mnara wa simu katika kijiji hicho.Kijiji cha Ifinga kinakabiliwa na changamoto ya kukosa miundombunu bora ya barabara hali ambayo inasababisha wananchi kulipia shilingi kati ya 40,000 hadi 70 kusafiri umbali wa kilometa 48.Kijiji hicho pia hakina mawasiliano ya simu.
PAROKO wa Parokia ya Ifinga Jimbo Kuu Katoliki la Songea Padre John Otete amesema kitendo cha jumuiya ya waumini wa parokia hiyo kuchangia shilingi milioni saba kwa ajili ya ukarabati wa kanisa hilo kumejenga na kufungua ukurasa mpya na hivyo kuachana na mawezo tegemezi ya kuwasaidia wahisani toka nje ya nchi kuwajengea makanisa.Kanisa katoliki la Mtakatifu Galus Parokia ya Ifinga Jimbo Kuu katoliki la Songea lilijengwa na wamisionari wa kijerumani mwaka 1932 hivi sasa lina miaka zaidi ya 90. Kanisa hili kongwe nchini linahitaji ukarabati kwa sababu hivi sasa baadhi ya kuta zake zimeweka nyufa pia linavuja hivyo linahitaji ukarabati mkubwa ili kuliokoa lisianguke.Paroko wa Parokia ya Ifinga Padre John Otete anawaalika watu wote wanauguswa kusaidiana na waumini wa Ifinga kuchangia ukarabati wa kanisa hili.Paroko anawaalika watu wote waliopo ndani na nje ya nchi kuchangia ukarabati wa kanisa hili iwe kwa fedha taslimu au vifaa.
NAIBU Waziri wa Madini Doto Biteko amefanya ziara katika machimbo ya Ngapa yaliyopo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kuzungumza na wachimbaji wadogo wanaochimba madini ya vito aina ya Gem Stone na kubaini wachimbaji wadogo wananyonywa na wafanyabiashara katika hali inayosikitisha. Imebainika kuwa baadhi ya wafanyabiashara wananunua madini hayo kwa bei ya chini ambapo wao wanakwenda kuyauza madini hayo mara 15 ya bei walionunulia.Wilaya ya Tunduru haijanufaika na madini tangu mwaka 1996,ambapo kwa mara ya kwanza imepata mapato ya madini katika mwaka 2017/2018 kwa kupata shilingi milioni 66,baada ya ya serikali kurekebisha sheria ya madini ambayo inamwezesha mtanzania kumiliki madini.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa