BENKI ya NMB taw la Songea mkoani Ruvuma imemaliza tatizo la madawati katika shule ya msingi Mipeta iliyopo kilometa 108 toka mjini Songea,baada ya kutoa mchango wa madawati 150 yenye thamani ya shilingi milioni 10.
BENKI ya NMB tawi la Madaba wilaya ya songea mkoani Ruvuma imetoa msaada wa viti 63 na meza 63 kwa ajili wanafunzi katika shule ya Sekondari Wino.Msaada huo umekabidhiwa na Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Frank Rutakwa ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya songea Pololet Mgema.
Katibu Tawala mkoani Ruvuma Profesa Riziki shemdoe ambaye amewakilishwa na Katibu Tawala Msaidizi Edimund Siame, amefungua Mafunzo ya kuibua na kubadilishana simulizi za mabadiliko kwa maafisa Habari,Elimu na wenyeviti wa waratibu kutoka Halmashauri zote nane za mkoa wa Ruvuma.Mafunzo ya siku mbili ambayo pia yamewashirikisha wanahabari toka vyombo mbalimbali vya habari yanafanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki Jimbo la Mbinga.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa