MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametoa maagizo mazito ya kuhakikisha Halmashauri zote zinakusanya mapato kwa asilimia 100 na kwamba Halmashauri ambayo itashindwa kufikia malengo atashauri ifutwe au kushushwa daraja.Mndeme alikuwa anazungumza na watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma mara baada ya kumuapisha Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo katika sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma mjini Songea.Sherehe hizo zimehudhuria na viongozi mbalimbali katika ngazi za wilaya na mkoa .
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amemwapisha mkuu wa wilaya Mpya wa Namtumbo Sophia Kizigo ili aweze kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wananchi wa Namtumbo.Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali ngazi za wilaya na mkoa
KATIBU Tawala mpya wa Mkoa wa Ruvuma Profesa Riziki Shemdoe amejitambulisha rasmi kwa watendaji wa wilaya na mkoa wa Ruvuma katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo ambapo ameweza kuvitaja vipaumbele vyake kuhakikisha Mkoa wa Ruvuma unasonga mbele.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa