UDANGANYIFU ni tendo lolote la uamuzi au uasi unaofanywa kwa lengo la kuwadanganya wengine na kusababisha anayedanganywa kupata hasara na anayedanganya kufaidika ama kwa kupata fedha.Akitoa mada ya vihatarishi vya udanganyifu kwa madiwani,wataalam na maafisa watendaji wa mitaa na Kata wa Manispaa ya Songea katika mafunzo ya siku mbili,Mkaguzi wa Ndani wa Manispaa hiyo Joel Mantakara anasema tendo la udanganyifu hujumuisha wizi,rushwa na njama.
Sergi Swai ni Mkaguzi wa Ndani katika Manispaa ya Songea mtazame akitoa mada ya viashiria hatarishi vya memejimenti kwa madiwani na watendaji wa Manispaa ya Songea, ameeleza viashiria hatarishi vya menejimenti uwezekano wa matukio kutokea ambayo yanaathari ya kutofikia malengo.Hata hivyo anasema viashiria hatarishi vinapimwa kwa athari na uwezekano wa kutokea.Anataja tofauti kati ya viashiria hatarishi na matatizo kuwa ni viashiria hatarishi sio uhakika na mabo yajayo ambayo yanaathari hasi na athari chanya katika kufikia malengo,ambapo matatizo ni utata,mzozo au migogoro baina ya pande mbili au Zaidi.
TAZAMA mabadiliko madogo ambayo yamefanywa na Rais Dkt.John Magufuli katika Baraza la Mawaziri na kufanya uteuzi wa makatibu wakuu na Naibu makatibu wakuu
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa