Mti unaoitwa Chikunguti,kitaalam dichrostachys cinerea wenye uwezo wa kuishi hadi miaka 1000 ni kivutio kingine cha utalii ndani ya makumbusho ya Taifa ya Majimaji yaliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma.
TAASISI na kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Ruvuma imewafikisha mahakamani watumishi sita wa umma kwa tuhuma za rushwa.Hayo yamesemwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoani Ruvuma Owen Jasson wakati anatoa taarifa ya utendajikazi wa Taasisi hiyo katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba 2018.
Mkuu wa wilaya ya Songea pololet Mgema amewaagiza wenyeviti wa serikali za mitaa katika Manispaa ya songea kuimarisha ulinzi na Usalama kuanzia ngazi ya mitaa.Mgema ametoa agizo hilo wakati anazungumza kwenye kikao ambacho pia kilishirikisha Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya Songea,Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea na maafisa watendaji wote wa mitaa 95 na kata 21 za Manispaa ya Songea.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa