IKIWA ni takribani wiki moja imepita hadi sasa tangu umeme wa Grid ya Taifa ulipowashwa katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amezidua kiwanda kipya kilichojengwa katika kata ya Ruhuwiko Manispaa ya Songea chenye uwezo wa kusaga mahindi tani 30 ambayo ni sawa na magunia 300 kwa siku.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji akizungumza katika mkutano wa Baraza maalum la madiwani wa Manispaa hiyo wenye lengo la kuwasilisha taarifa za Hesabu za kufunga mwaka 2017/2018,amesema kiwanda hicho kimezinduliwa wakati muafaka kwa sababu hivi sasa kitapunguza changamoto za soko la mahindi katika manispaa ya Songea na mkoa wa Ruvuma na kutoa ajira kwa vijana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli akizungumizia muhimu wa halmashauri zote nchini kusimamia mapato. Magufuli amesishia Halmashauri ambazo zinashindwa kukusanya kodi kushishwa hadhi.
Watazame maafisa ngazi ya wilaya zote za mkoa wa Ruvuma wakipata Mafunzo ambayo yameendeshwa na TUSOME PAMOJA Kwa lengo la kuwajengea uwezo katika simulizi za mabadiliko.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa