MTAZAME Mwekazina Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Denis Mwaitete akizungumzia Manispaa ya Songea ilivyofanikiwa kufuatia ripoti a Mkuaguzi Mkuu wa mahesabu ya serikali CAG.Mwaitete ametoa taarifa hiyo kwenye kikao maalum cha kujibu hoja za ukaguzi kilichofanyika kwenye ukumbi wa manispaa ya Songea
MTAZAME Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Alhaji Abdul Hassan Mshaweji akizungumzia mafanikio ambayo manispaa hiyo imeyapata ikiwemo kupata Hati safi mfululizo kufuatia ukaguzi wa mahesabu ambao umefanywa na CAG.Mshaweji alikuwa anazungumza katika kikao maalum cha kujibu hoja kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme
WAUMINI wa Kanisa katoliki Parokia ya Ifinga Jimbo Kuu katoliki la Songea wamechangia zaidi ya shilingi milioni saba kwa ajili ya ukarabati wa kanisa la parokia hiyo ambalo linahitaji zaidi ya shilingi milioni 68 kufanikisha ukarabati huo.Akitangaza fedha zilizopatikana katika harambee iliyofanyika katika kanisa la Mtakaifu Galus Ifinga,mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Madaba ambaye aliwakilishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Vestus Mfikwa,alisema kati ya fedha hizo pesa taslimu ni shilingi milioni 3.39 na ahadi ni shilingi milioni 3.6.Kanisa katoliki la Mtakatifu Galus Parokia ya Ifinga Jimbo Kuu katoliki la Songea lilijengwa na wamisionari wa kijerumani mwaka 1932 hivi sasa lina miaka zaidi ya 90. Kanisa hili kongwe nchini linahitaji ukarabati kwa sababu hivi sasa baadhi ya kuta zake zimeweka nyufa pia linavuja hivyo linahitaji ukarabati mkubwa ili kuliokoa lisianguke.Paroko wa Parokia ya Ifinga Padre John Otete anawaalika watu wote wanauguswa kusaidiana na waumini wa Ifinga kuchangia ukarabati wa kanisa hili.Paroko anawaalika watu wote waliopo ndani na nje ya nchi kuchangia ukarabati wa kanisa hili iwe kwa fedha taslimu au vifaa.Makadirio ya ukarabati ni fedha za kitanzania shilingi milioni 68.Unaweza kuchangia kupitia akaunti ya Benki au Simu kama ifuatavyo:1.JINA LA AKAUNTI:PAROKIA YA MTAKATIFU GALUS IFINGAJINA LA BENKI:NMB TAWI LA SONGEANAMBA YA AKAUNTI:618100352662.MWENYEKITI WA KAMATI UCHUMI NA UJENZI PAROKIA YA IFINGA MR.KINEMO KIHOMANOMPESA 07543349343.MHASIBU MR.GEBHARD NYONIMPESA 07540231154.PAROKO WA PAROKIA YA IFINGA PADRE JOHN OTETEMPESA 0756313380KUTOA NI MOYO,CHANGIA KAZI YA MUNGU,WOTE MNAKARIBISHWA.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa