Tazama namna siku ya tembo ilivyoadhimishwa katika Mkoa wa Ruvuma ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme.
September 27, 2018 ni siku ya 8, tangu kuzama kwa meli ya Mv. Nyerere na hadi leo ni siku 4, tangu zoezi la kukinasua Kivuko kutoka ndani ya maji lianze linaongozwa na Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo.
Luteni Kanali Mstaafu Daniel Gangisa (90) ni mmoja wa Brigedi Kamanda aliyeongoza vikosi kumng,oa Dikteta Idd Amini Dada katika ardhi ya Tanzania hadi Uganda mwaka 1979.Shujaa wa Tanzania,Gangisa ni Mstaafu wa JWTZ ambaye anaishi katika Kitongoji cha Chandarua Kata ya Mshangano Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma.
Gangisa alisoma na Idd Amini nchini Kenya kuanzia mwaka 1953,1954 hadi mwaka 1955 ,waliishi bweni moja ,chumba kimoja na kulala kitanda cha double decker mmoja chini na mwingine juu.walikutana tena na Idd Amini mwaka 1960 Nakuru nchini Kenya.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa