MKUTANO wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma limeunga mkono kusitisha nia ya kuanzisha Bodi ya Mfuko wa Elimu katika Manispaa hiyo.Wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea chini ya Mwenyekiti Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Alhaj Abdul Hassan Mshaweji,wajumbe wameunga mkono uamuzi huo.Mapendekezo ya kutunga sheria ya uanzishaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu katika Manispaa ya Songea yalifutwa tangu Julai 16 mwaka huu kutokana na mapendekezo hayo kutokubalika na wananchi ikiwemo ada ya shilingi 10,00 kwa mwaka kuchangiwa na kila mwananchi.
MKUTANO wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma limeunga mkono kusitisha nia ya kuanzisha Bodi ya Mfuko wa Elimu katika Manispaa hiyo.Kwa upande wake Diwani Chikwale anasisitiza kuwa rasimu hiyo imeleta usumbufu mkubwa kwa wananchi katika kata na mitaa na kwamba wanawaona kwamba madiwani wameshindwa kuwatetea wananchi.
KAKAKUONA ambaye ni mnyama adimu duniani leo amezua amekuwa kivutio cha aina yake katikaviunga vya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ,baada ya watu mbalimbalikujitokeza kumshangaa mnyama huyu. Jina kakakuona linatokana na uadimu wake wa kutokuoneka,mnyama huyu huchukuliwa kwamba kuonekana kwake ni bahati kwa namna moja au nyingine.
Soma zaidi hapahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mambo-13-usiyoyajua-kuhusu--kakuoana/1597296-2611258-ch9dblz/index.html
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa