Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imetembelea mradi wa ujenzi wa lami nzito katika Manispaa ya Songea zenye urefu wa kilometa 10.3 unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 10.Mradi unaotarajia kukamilika Septemba 30,umefikia asilimia 72.
MRADI wa ujenzi wa kivuko kinachounganisha kata za Lizabon na Ruhuwiko Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma umefikia asilimia 80.
Mhandisi wa Ujenzi katika Manispaa hiyo Mhandisi Nicholus Danda amesema mradi wa kivuko hicho hadi kukamilika utagharimu sh.milioni saba ambapo hadi sasa zimetumika sh.milioni tano.Mradi huo wa mwezi mmoja,ulianza Juni 3,2019 na unatarajia kukamilika Julai 3,2019.
SERIKALI imetoa zaidi ya shilingi milioni 950 kwa ajili ya kukarabati sekondari kongwe ya Songea Boys ambayo ilianzishwa mwaka 1950 na serikali ya wakoloni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa