VIPIMO vya maabara vya mkemia mkuu vinaonesha kuwa kiwango cha sumu ya zebaki katika bandari ya Ndumbi ziwa Nyasa mkoani Ruvuma kimezidi mara tatu ya kiwango cha kawaida hali ambayo inatishia maisha ya watu na viumbehai vya majini.Akitoa ripoti ya ukaguzi kwa wataalam wa maji na mazingira wa Mkoa wa Ruvuma,kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea ,Mratibu wa Baraza la Taifa la Kudhibiti Mazingira(NEMC) Kanda ya Kusini, Lewis Nzali amesema vipimo vya kikemia vilivyochukuliwa katika bandari ya Ndumbi vinaonesha kuwa sumu ya zebaki imefikia 0.018Hg wakati kiwango kinachotakiwa ni 0.005Hg
MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo wametiliana Mkataba wa lishe katika Manispaa ya Songea ambao utadumu kwa miaka minne kuanzia Julai 2018 hadi Juni 30,2021
SHIRIKA lisilo la kiserikali la TUSOME PAMOJA kwa kushirikiana na serikali limechochea kupunguza changamoto ya wanafunzi kutojua KKK katika shule za msingi za Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Fuatilia makala haya
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa