Wanafunzi wa darasa saba katika nchi nzima wanafanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba kwa siku mbili ambazo ni Septemba 5 na 6,2018.Kama anavyobainisha Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt.Charles Msonde
MMOJA wa wanamuziki wa kizazi kipya katika Manispaa ya Songea ZM akitumbuiza kwenye kampeni za Furaha Yangu ngazi ya Mkoa wa Ruvuma ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
Rais Magufuli amekemea vitendo vya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria huku akiunga mkono jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina katika kukabiliana na tatizo hilo. Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye viwanja vya Ukuta mmoja Mjini Nansio, wilayani Ukerewe, Rais Magufuli ameeleza kwa kina madhara ya uvuvi huo huku afichua kuhusu kilichofanya meli ya uvuvi iliyowahi kukamatwa katika Bahari ya Hindi, izame.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa