Ujenzi wa awamu ya kwanza wa reli ya kisasa(SGR) umefikia asilimia 16,ukitarajiwa kukamilika Novemba mwaka huu.Reli hiyo itatumiwa na Reli yenye kasi ya kilometa 160 kwa saa na uendeshaji wake utakuwa wa umeme na mafuta
HIFADHI ya Taifa ya wanayama pori ya Serengeti nchini Tanzania imeibuka ya kwanza Afrika baada ya utafiti uliofanywa na kampuni ya utalii ya Safari Bookings, utafiti uliofanyika mtandaoni kupitia tovuti yake.
Hifadhi hiyo imepata alama 4.9 kati ya 5. Mwaka 2015 Serengeti ilishinda na kuwa hifadhi bora zaidi.Moja ya sababu za hifadhi hiyo kuwa bora zaidi ni uwepo wa wanyama wengi wakiwemo aina tano kubwa (Big Five) ambao ni Tembo, Simba, Faru, Chui na Nyati.Sababu nyingine ni kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni limetaja eneo hilo kuwa urithi wa dunia.
MWENYEZI Mungu kila kiumbe amempa uwezo wa kupambana na maadui hata kuweza kujipatia ridhiki yake.Hebu tazama maajabu ya kiumbe hiki kidogo sana ambacho unaweza kukiua kwa vidole kilivyofanikiwa kumwangamiza nyoka na kujipatia kitoweo
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa