MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amekagua mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya kata yake, Ruvuma manispaa ya Songea na kiridhishwa na kasi ya ujenzi wake .Ujenzi wa Kituo hicho ambacho serikali imetoa shilingi milioni 400, umeanza Septemba mwaka huu.
MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amekabidhi msaada wa magodoro,vitanda na mashuka nyenye thamani ya shilingi milioni tano ambavyo vimetolewa na Benki ya NMB katika Kituo cha Afya Madaba kilichopo katika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
WANANCHI wa Kata ya Lilambo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanatarajia kunufaika na mradi wa maji ya mtiririko wenye thamani ya shilingi bilioni 1.1,mradi ambao unatarajia kukamilika Juni 30,2019.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa