RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli amekubali ushauri wa viongozi wastaafu wakiwamo Marais wastaafu,mawaziri wakuu na majaji wastaafu ambao aliwaalika Ikulu jijini Dar es salaam.
OFISI ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imetoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya ukarabati wa madarasa manne ya shule ya msingi Chandamali.Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Keziah Katawa amesema shule hiyo,Desemba 2017 ilipata maafa ya kuezuliwa kwa paa la madarasa manne na ofisi mbili.
TANZANIA ni miongoni mwa nchi chache duniani ambayo ina fursa za kipekee ambazo zinaweza kuchochea utalii wa ikolojia kupitia ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa.
Maziwa hayo mawili yanatajwa kuwa na aina mbalimbali za samaki wa mapambo ambao baadhi yao wana sifa ya kutoa umeme hivyo wamepewa jina la samaki umeme(electric fish).
Utafiti wa awali ambao ulifanywa katika ziwa Tanganyika na Mwanasayansi Erick Fortune kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha nchini Marekani unaonesha kuwa samaki-umeme wana uwezo wa kutoa umeme kwa kutumia ogani umeme iliyopo kwenye mikia ya samaki hao.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa